Be the
Pride

Idadi ya simba iko hatarini, na wewe ndiyo suluhisho.

Saidia Sasa
Picha na Chris Schmid

Kihistoria, simba walipatikana maeneo mengi Africa, leo wametoweka kutoka katika 94% ya maeneo hayo.

010203040506/06

Kwa Nini Tunawahitaji Simba

Kuwaokoa simba ni jambo zuri kwa uchumi wetu, mazingira yetu na sisi.

Chukua
Hatua

Njia bora zaidi ya kuchukukua hatua ni kuwatumia viongozi, wenye ushawishi na wenyeuamuzi Tanzania, ujumbe kwa kupitia mtandao wa kijamii wa twitter usemao #bethepride okoa simba kabla hawajatoweka kabisa. Anza kwa kubofya kwenye akaunti iliopo hapo chini.

Sambaza Video
"Simba Ni"

Simba ana maana gani kwako?

Nchini Tanzania, simba ni ishara ambayo imeingiliana sana na utambulisho wetu wa taifa, ikiwakilisha sio tu urithi wetu mkubwa wa asili, ila pia tabia tunazothamini na kuvaa kama taifa. Sifa kama nguvu, fahari, mamlaka, ujasiri na ustahimilivu. Ili kuongeza ufahamu juu ya kiasi gani simba ameingiliana sana na utambulisho wetu, tafadhali sambaza video ya Simba Ni. Kisha soma kuhusu watu wenye uhamasisho walioko kwenye video kwa kubofya kwenye wasifu wao.

Kuhusu watu

Mrisho Mpoto

Mshairi na Msanii

Mrisho Mpoto

Mrisho ni mshairi, mwigizaji, muongozaji na msimulizi maarufu, ambaye ana mapenzi makubwa na uigizaji wa mashairi ya Kiswahili. Kwa kuwa amekuwa na mapenzi makubwa na mazingira tangu akiwa mdogo, Mrisho ameamini kwa muda mrefu kuwa vitu vyote vya asili vinahitaji kulindwa na kutunzwa kwa upendo na kwa sababu hii ametunga nyimbo nyingi kuhusu thamani ya mazingira na athari za ujangili, ikiwemo wimbo maarufu uitwao "Deni la Hisani".

Mashujaa wa Uhifadhi Wasiojulikana

Kusherehekea watu wanaoleta mabadiliko.

Yamat Lengai

Monitoring and Evaluation Officer

Stefano Asicheka

Community Liaison Officer

Neria Abdi

Lion Conflict Officer

Mandela and Julius

Lion Defenders

Bernard Kissui

Lion Researcher

Yamat. Neria. Julius. Mandela. Bernard. Stefano. Kirerenjo. Unaweza usitambue majina haya, lakini hawa ni mashujaa wetu na tunatumaini watakuwa wa kwako- wao ni wanaume na wanawake wa kawaida wanaofanya kazi mchana (na wakati mwingine usiku) kwenye uhifadhi wa wanyamapori, wakichangia juhudi zao katika kulinda simba wa Tanzania na mazingira yao. Mfululizo wetu unaowamulika Mashujaa wasiojulikana wa Uhifadhi unawatambua watu ambao mara nyingi hawajulikani na hawaonekani mara kwa mara ambao wana nafasi kubwa sio tu katika kuhifadhi spishi hii pendwa ila pia katika kusaidia jamii ambazo zinapitia changamoto ya kuishi karibu nao.

Inaweza kuwa watetezi wa simba kama Julius na Mandela, waliofanya kazi kuzuia uwindaji wa kiasili wa simba, au mama anayefanya kazi, Yamat, anayekusanya habari za thamani sana zinazolisaidia shirika lake kufanya maamuzi yenye ufanisi ya kuzuia mashambulizi ya simba; au Kirerenjo, anayeelimisha wafugaji kuhusu kuchunga wanyama wao kwa ufanisi zaidi na kwa njia yenye madhara madogo zaidi kwenye makazi ya simba. Tafadhali tazama film zetu za mashujaa wa uhifadhi alafu uwaachie ujumbe wa kuwatia moyo.

Simba

Simba
Maishani Mwangu

Tunauona mchoro wa simba kila mahali, kuanzia noti za fedha mpaka kanga, fulana na mapambo. Ni ishara muhimu, sehemu ya historia yetu na simulizi, imekuwa ni sehemu kubwa sana ya utamaduni wetu mpaka mara nyingi hata hatuitambui. Ila sasa tunakutaka utuonyeshe uwepo katika maisha yako wa huyo simba aliyepuuzwa na kusahauliwa kwa muda mrefu kwa kupiga picha wakati wowote unapoona kitu chenye nembo au picha ya simba – inaweza kuwa kishikio cha ufunguo, mchoro, bango, fulana, hata tatoo! – na upakie kwenye Instagram ukitumia alama za reli (hashtags) #lioninmylife na #bethepride.

Tuambie kwa sentensi moja simba ana maana gani kwako na utaingizwa kwenye droo. Mshindi atapata safari iliyogharamiwa kwa kila kitu ya kwenda Serengeti Tanzania kuwaona simba katika mazingira yao halisi, ambapo utalipiwa kukaa katika hoteli nzuri ya Alex Walker Serian iitwayo Serengeti Lamai. Ili kuangalia vigezo na masharti, tazama hapa.

Instagram post
Instagram post
Instagram post
Instagram post
Instagram post
Instagram post
Instagram post
Instagram post
Instagram post

Washirika